Hivi karibuni kundi la sanaa ya uigizaji la Orijino komedi liliingia matatani baada ya Jeshi la Polisi kanda maalum ya Dar es salaam kuwahoji wasanii wanne wa kundi hilo kwa tuhuma za kuvaa sare za polisi kwenye harusi ya msanii Emmanuel Mgaya maarufu kama Masanja ambapo waliachiwa kwa dhamana.
August 22 2016 kupitia taarifa ya habari ya Azam, mmoja ya wachekeshaji hao Isaya Gidion ‘Wakuvanga’ amehojiwa na kusema…
‘mara zote huwa tunawasiliana nao kabla ya kufanya lakini kwa kipindi hiki tulisahau, na kwa kusahau kwetu ndio yakatoa yale lakini hatukuwa na maana mbaya kwamba tunadharau jeshi la polisi’
Video: