SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Jumatatu, 18 Aprili 2016

T media news

Wanachama 4 wa chama tawala Burundi wauawa

Afisa mmoja wa Burundi amesema kuwa wanachama wanne wa chama tawala cha nchi hiyo wameuawa kwenye shambulio katika ghasia zinazoendelea kuhusiana na kurefushwa muhula wa kusalia madarakani Rais Pierre Nkurunziza wa nchi hiyo.

Jerome Ntakarutimana Mkuu wa wilaya ya Mugamba mkoani Buriri amsema kuwa shambulio hilo lilifanywa kwa wafuasi wa chama tawala cha Burundi ambao walikuwa wamekusanyika kwa ajili ya shughuli ya kusafisha mazingira. Mtu mwingine aliyenusrika na shambulio hilo amesema kuwa wanachama hao wanne waliaga dunia baada ya watu wenye silaha waliovalia sare za jeshi kushambulia baa moja juzi Jumamosi na kufyatua risasi. Shambulio hilo limeifanya idadi ya watu waliouliwa Burundi tangu wiki iliyopita kufikia kumi.

Hatua ya Nkurunziza ya kugombea kiti cha urais kwa muhula wa tatu imesababisha machafuko ya kisiasa Burundi ambapo hadi sasa raia wa nchi hiyo zaidi ya 400 wameuawa