SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Jumatatu, 21 Machi 2016

T media news

Obama afanya ziara ya kihistoria Cuba

 Obama amesema ziara yake itatoa nafasi ya ushirikiano zaidi

Rais wa Marekani Barack Obama ameanza ziara ya kihistoria nchini Cuba, akiwa ndiye rais wa kwanza wa Marekani kuzuru taifa hilo katika kipindi cha miaka 88.

Ziara hii ya siku tatu ndiyo kilele cha mazungumzo ya miaka miwili yaliyonuia kurekebisha uhusiano kati ya Marekani dola kubwa zaidi duniani na jirani yake yenye mfumo wa ujamaa.

Rais Obama atakutana na Rais Raul Castro. Punde baada ya kuwasili Obama alitembea kwenye barabara za mji wa kale wa Havana na pia kuwahutubia wafanyikazi wa ubalozi mpya wa Marekani.

Obama apungia watu mkono baada ya kuwasili

Kiongozi huyo amesisitiza ziara yake inatoa nafasi kushauriana na raia wa kisiwa hicho.

Pia ameahidi kuangazia masuala ya haki za binadamu, kuwepo mageuzi ya kisiasa japo maafisa wa Cuba wamesema hakuna ajenda ya kujadili vile nchi hiyo inaweza kukubalia vyama vingi vya kisiasa. Cuba inataka zaidi kuondolewa vikwazo vyote vya kiuchumi na Marekani.

Baada ya kuwasili Cuba, Rais Obama aliandika kwenye Twitter akiwasalimu raia wa Cuba na kusema anasubiri kukutana nao na kusikia kutoka kwao.