SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Jumamosi, 12 Machi 2016

T media news

Tetesi: Kanye West Afukuzwa Kwenye Nyumba ya Mama Mkwe Wake...Yadaiwa Tabia Mbaya Imemponza


Mama yake na Kim Kardashian, Kris Jenner anadaiwa kuchoshwa na tabia mbaya ya Kanye West kiasi cha kumfukuza kwenye nyumba yake.

“Kris na Kanye walikuwa na mabishano makali,” chanzo kililiambia Touch.

Mgogoro huo ulianza baada ya Kanye kutaka kuharibu dili la binti wa Kris, Kylie na Puma. Kanye alidaiwa kumlaumu Kris kwa kuchukulia kuwa walimsaliti sababu ya uhusiano wake na Adidas.

Kwa mujibu wa RadarOnline, Kim na Kanye wamekuwa wakiishi kwenye nyumba ya mama yao wakati wakiendelea na ukarabati wa nyumba yao.

Inasemekana kuwa baada ya kutimuliwa, Kanye alienda kuishi kwa Jay Z na Beyonce.