SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Jumatatu, 28 Machi 2016

T media news

Sudan yasaini mkatana UN wa kulinda watoto


Sudan yasaini mkatana UN wa kulinda watoto
Serikali ya Sudan imetia saini hati ya Umoja wa Mataifa ya Kulinda watoto.
Taarifa iliyotolewa leo na Umoja wa Mataifa imesema kuwa, serikali ya Sudan imesaini hati ya umoja huo inayosisitiza udharura wa kulindwa watoto.
Wakati huo huo Waziri wa Ustawi wa Jamii wa Sudan, Ibrahim Adam Ibrahim amethibitisha habari hiyo na kusema kuwa, serikali ya Khartoum itafanya kila iwezalo kulinda haki za watoto katika maeneo yanayokabiliwa na hatari na mapigano ya ndani. Adam ibrahim ameongeza kuwa, serikali ya Sudan pia itaimarisha zaidi taratibu za sheria ya kulinda watoto iliyopasishwa mwaka 2010 na sheria ya vikosi vya jeshi la nchi hiyo.
Kwa mujibu wa hati hiyo serikali ya Sudan italazimika kuunda timu ya kushughulikia masuala ya haki za watoto ikishirikiana na Umoja wa Mataifa.