SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Jumatatu, 28 Machi 2016

T media news

Ripoti mpya imeonyesha kuwa mamilioni ya wananchi wa Uganda wanakabiliwa na baa la njaa.


Ripoti: Waganda milioni 4 wanakabiliwa na baa la njaa
Ripoti mpya imeonyesha kuwa mamilioni ya wananchi wa Uganda wanakabiliwa na baa la njaa. Asilimia 11.8 ya Waganda, ambayo ni zaidi ya watu milioni 4 wanakabiliwa na baa la njaa kutokana na umaskini na ugumu wa maisha.
Ripoti ya matokeo ya sensa ya mwaka 2014 iliyozinduliwa hivi karibuni na Rais Yoweri Museveni wa nchi hiyo imeonyesha kuwa, mamilioni ya Waganda hawawezi kumudu milo miwili kwa siku na hivyo wanalazimika kupata mlo mmoja tu. Ripoti hiyo imebainisha kuwa, asilimia 51.4 pekee ya wananchi wa nchi hiyo ya Afrika Mashariki sawa na Waganda milioni 18 ndio wanaweza kupata milo miwili kwa siku na kwamba asilimia 34.6 ndio wanaopata milo mitatu kwa siku.
Aidha ripoti hiyo iliyozinduliwa wiki iliyopita imesema kuwa, takriban Waganda milioni 18 wanatumia mafuta taa kwa ajili ya kupata mwangaza, jambo ambalo linawaweka katika hatari ya kukumbwa na saratani ya mapafu.
Kadhalika imebainisha kuwa asilimia 27.2 ya wananchi wa Uganda wanaishi katika hali ngumu ya maisha vijijini na kwamba asilimia 7.4 pekee ndio wanaoishi mijini.