Msomi mmoja kutoka Tanzania Aneth David Mwakilili ni miongoni mwa wasomi wengine walioteuliwa kuwania tuzo la wanasayansi wachanga barani afrika maarufu kama The Next Einstein Forum (NEF).
Tuzo hiyo huleta pamoja wasomi wa sayansi, watunga sheria na washika dau katika seKta mbali mbali barani afrika, kujadili na kuhimiza sayansi inayoweza kutatua matatizo yanayokumba bara la Afrika.
Washindi wa tuzo hiyo wanapewa ufadhili na usaidizi kutoka kwa wakfu huo ili kutekeleza utafiti wao kikamilifu.
Katika shindano hili Mwakilili, atafanya utafiti ambao utasaidia wakulimu kutokomeza kwekwe na hivyo kuimarisha mazao yao.