SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Ijumaa, 11 Machi 2016

T media news

Bob Junior Akamatwa na Polisi Kwa Tuhuma za Kushirikiana na Majambazi


Msanii wa muziki wa bongo fleva Bob Junior amekamatwa na jeshi la Polisi nyumbani kwao magomeni mapipa Jijni Dar es salaam majira ya saa sita mchana wa leo.

Kwa mujibu wa chanzo cha  habari ambaye ni rafiki wa karibu wa Bob Junior ameiambia Mtembezi.com kuwa Polisi wamemkamata Msanii huyo kwa kile walichodai kuwa wamepata taarifa kuwa Bob Junior anashirikiana na kikundi cha majambazi.

Rafiki huyo wa karibu na Bob Junior, ameiujuza mtembezi.com kuwa Msanii huyo amekuwa akipigiwa simu tangu juzi kutoka kituo cha polisi cha magomeni usalama kwamba kuna lalamiko la mtu anaye dai kutekwa na kikundi cha majambazi ambacho msanii huyo anashirikiana nacho.