Ritha alisema kutokana na wingi wa ving’amuzi kwa sasa, uhitaji wa vipindi vya nyumbani ni mkubwa, hivyo wasanii na maprodyuza wa video wanatakiwa kutumia fursa hizo ili kujipatia fedha na kukuza uchumi wao.
“Huu ni muda muafaka kwa wasanii wa ndani kufanya ‘production’, kwa kuwa ving’amuzi vipo vya kutosha na vituo vya runinga vinatafuta ‘local content’,’’ alieleza Madam Ritha.
Katika hatua nyingine, msanii anayetamba na wimbo wa ‘Katoto’, Kayumba Juma, amemshukuru Madam Ritha na kampuni yake kwa kufanikisha video ya wimbo wake huo kama walivyokubaliana awali.
“Kulikuwa na mikataba lakini nashukuru wamenifanyia kazi yangu ambayo kwa sasa napita nayo kifua mbele na naamini itaniweka sehemu nyingine na kazi yote hiyo amefanya Madam Ritha na sasa kazi zangu zinasimamiwa na Mkubwa Fella, ambaye anahakikisha najulikana na nyimbo zangu zinafika mbali,’’ alieleza Kayumba.