SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Jumamosi, 12 Machi 2016

T media news

JOYCE KIRIA Amchimba Mkwara Mume Wake...Atishia Kumpiga Chini Asipofanya Haya


Mtangazaji wa Kipindi cha ‘Wanawake Live’ kinachorushwa kupitia Televisheni ya East Africa, Joyce Kiria amefunguka kuwa hata kama mumewe wa ndoa hatakuwa mchapakazi atampiga chini na kuendelea na maisha mengine.

Akizungumza na mwandishi wa habari, Joyce, ambaye leo anazindua rasmi kampeni yake ya ‘Mwanamke Piga Kazi’ inayofanyika katika Viwanja vya Leaders jijini Dar, alisema kuwa kwa kipindi ambacho tupo nacho sasa hivi lazima kupiga kazi.

“Kwangu, hata kama mume naye atakuwa mzembe wa kupiga kazi nampiga chini kabisa maana sasa hivi tunakimbizana na kazi ya kupiga kazi kwa nguvu ili tuwezeshe kusonga mbele zaidi,”  alisema Joyce.

Pia mtangazaji huyo aliongeza kuwa anawaomba wanawake wengi wajitokeze kwani hakutakuwa na kiingilio chochote, lengo ni kuja kujifunza mbinu za kujikomboa kama wanawake na kujiamini katika kufanya kazi.