SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Jumamosi, 12 Machi 2016

T media news

Katibu Mkuu Mpya CHADEMA Huyu Hapa!


Wananchi hapa wanasubiri ujio mkuu leo.Ujio wa Katibu mkuu wa Chama chenye ufusi mkubwa nchini cha Chadema.

Kiongozi mkuu wa upinzani nchini Freeman Mbowe ndiye atakayesimama leo mbele ya Baraza Kuu kutegua kitendawili kinachosubiriwa kuteguliwa na mamilioni ya wafuasi ndani na nje ya nchi.

Tayari majina kadhaa yasiyopungua kumi yamekuwa yakibashiriwa kwamba moja kati ya hilo ndilo litakalopita katikati ya moshi mweupe pale kwenye ukumbi wa Gold Crest.

Hekima na busara nyingi za Freeman Mbowe zimesababisha mpaka leo jina hilo kuwa siri kuu.Hata hivyo uchunguzi wa kuaminika kutoka kwa watu wa karibu na washauri wakuu wa Freeman Mbowe unasema Katibu mkuu mpya atakuwa ni mpenda chama na wananchi,kiongozi asiyeyumbishwa,mtetezi wa Katiba ya chama na jasiri asiyeyumbishwa atakayekuwa na uwezo wa kutamka jambo na nchi inasimama.

Waandishi wa habari wa ndani na nje ya nchi wamefurika kwenye viunga vya ukumbi huu kujiandaa kuwa wa mwanzo kurusha jina la Katibu mkuu mara litakapotangazwa.

Tunatarajia kabla siku ya leo kuisha tuwawekee hapa jina la Katibu Mkuu mpya Chadema mara baada ya Moshi mweupe kuonekana.