SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Jumamosi, 12 Machi 2016

T media news

Karatasi za kupigia kura zawasili visiwani Zanzibar

     
Karatasi za kupigia kura zawasili visiwani Zanzibar
Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar nchini Tanzania jana ilipokea shehena ya karatasi zitakazotumika kwa ajili ya kupigia kura katika uchaguzi mkuu wa marudio unaotarajiwa kufanyika Machi 20 mwaka huu katika visiwa hivyo.
Makaratasi hayo yaliyochapishwa nchini Afrika Kusini yaliwasili jana na kupokewa na Tume ya Uchaguzi Zanzibar ZEC huku tume hiyo kitangaza kuwa maandalizi yote ya uchaguzi huo yamekamilika na kwamba, uchaguzi huo wa marudio utagharimu kiasi cha shilingi bilioni 4.5. Karatasi hizo zina picha za wagombea wote 14 wa kiti cha Urais wa Zanzibar licha ya baadhi ya wagombea akiwemo wa CUF Maalim Seif Sharif Hamad kutangaza kwamba, hatagomnea katika uchaguzi huo wa marudio.
Zanzibar ambayo ni sehemu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania iliingia katika mgogoro wa kisiasa mwezi Oktoba mwaka jana baada ya Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi visiwani humo Jecha Salim Jecha kufuta matokeo ya uchaguzi kwa kile alichokiita ukiukwaji wa sheria na utaratibu wakati wa zoezi la upigaji kura.
Uchaguzi wa marudio Zanzibar unatarajiwa kufanyika tarehe 20 ya mwezi huu wa Machi huku vyama tisa kati ya 14 vilivyoshiriki katika uchaguzi uliofutwa wa Oktoba 25, kikiwemo chama cha CUF ambacho kinadai mgombea wake wa urais Maalim Seif Sharif Hamad ndiye mshindi halali wa kiti hicho vikiwa vimeshatangaza rasmi kwamba, havitashiriki katika uchaguzi huo.