SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Jumamosi, 12 Machi 2016

T media news

UN yalaani ukiukwaji wa haki za binadamu S/Kusini

UN yalaani ukiukwaji wa haki za binadamu S/Kusini
UN yalaani ukiukwaji wa haki za binadamu S/Kusini
Ofisi ya Haki za Binadamu ya Umoja wa Mataifa imelaani vikali uvunjaji mkubwa wa haki za binadamu nchini Sudan Kusini na kusema kuwa, askari wa serikali wamefanya jinai za kibinadamu nchini humo.
Ofisi ya Haki za Binadamu ya Umoja wa Mataifa ilitoa taarifa hiyo jana (Ijumaa) na kusema kuwa, uvunjaji wa haki za binadamu nchini Sudan Kusini ni sawa na jinai za kivita.
Zeid Raad al-Hussein, Kamishna wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa ameongeza kuwa, uvunjaji wa haki za binadamu nchini Sudan Kusini ni mbaya na mkubwa mno kuliko sehemu yoyote ile duniani.
Katika ripoti yake kuhusu Sudan Kusini, Umoja wa mataifa umesema kuwa, picha zilizopigwa na satalaiti zinaonesha namna miji na vijiji vya nchi hiyo vinavyoharibiwa kwa makusudi.
Umoja huo umesema, uhalifu wa kijinsia huko Sudan Kusini nao ni wa kutisha na umelitaka Baraza la Usalama la umoja huo lifungue mashtaka katika Mahakama ya Kimataifa ya Jinai ICC ili ifuatilie uhalifu huo.
Katika upande mwingine, shirika la haki za binadamu la Amnesty International limesema kuwa askari wa serikali walirundika watu kwenye kontena moja na kupelekea zaidi ya watu 60 kupoteza maisha kwa kukosa pumzi.