SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Jumamosi, 12 Machi 2016

T media news

Rais Dos Santos: Karibu nitaondoka madarakani

     
Rais Dos Santos: Karibu nitaondoka madarakani
Rais Jose Eduardo Dos Santos wa Angola amesema kuwa, ataondoka madarakani mwaka 2018.
Rais Dos Santos ameyasema hayo Ijumaa wakati akihutubia wajumbe wa chama chake cha MPLQ na kuongeza kuwa ifikapo mwaka 2018 ataondoka madarakani baada ya kumalizika mihula yote ya uongozi wake.
Muhula wa uongozi wa Rais Jose Eduardo Dos Santos aliyeingia madarakani tangu mwaka 1979, unatazamiwa kumalizika mwaka 2017.
Chama tawala nchini Angola tayari kimeanzisha vikao kwa ajili ya kumuainisha mtu atakayerithi nafasi ya rais huyo.
Hayo yanajiri katika hali ambayo marais wengine wa Afrika wamekuwa wakikataa kuondoka madarakani licha ya katiba za nchi zao kuwabana kufanya hivyo.