Maafisa wawili nchini Burundi wamejikuta wakitupwa gerezani baada ya kumchezea rafu Rais wa nchi hiyo, Pierre Nkurunziza katika mechi ya kirafiki iliyokuwa imeandaliwa.
Mechi hiyo iliyochezwa Februari 3, mwaka huu baina ya timu aliyokuwa akiichezea Rais Nkurunzinza ya Haleluya FC dhidi ya timu ya mji ulioko mji wa Kaskazini wa kiremba.
“Kwa kawaida, timu ya upinzani ilijua kuwa inacheza dhidi ya Rais, na ilitakiwa wasikaze sana na pengine ni ili kumruhusu afunge magoli. Lakini kwa kuwa timu hiyo iliundwa na wachezaji wengi ambao ni wakimbizi kitoka Congo, hawakujua kama wanacheza na Rais wa nchi hiyo. Walimkaba kila mara alipopata mpira kitu kilichomfanya aanguke mara kwa mara” alisema mmoja wa mashahidi.
Kufuatia tukio hilo, viongozi wawili wa timu ya Kiremba walihukumiwa kifungo jela siku ya Alhamisi, Machi Mosi mwaka huu.
Viongozi hao walihukumiwa kwa kosa ambalo lilitajwa kuwa ni “Kuunda njama dhidi ya Rais”.
Chanzo: BBC