SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Ijumaa, 23 Machi 2018

T media news

VIONGOZI WENGI WA KIAFRIKA HAWAHESHIMU AKILI KUBWA.


Na Thadei Ole Mushi.

#Siku Za Karibuni Julias Malema aliulizwa swali na mwandishi mmoja kama ana ndoto za kuja kuwa Rais Wa Afrika Kusini. Jibu lake alilojibu alisema "Any Fool can be a president" Mjinga yeyote anaweza akawa Rais. Malema alendelea kusema kuwa hata kama RAIS ni mjinga kiasi gani anaweza kufanya kazi zake vizuri sana kama atazungukwa na watu wenye akili. Malema alimtolea mfano Donald Trump kuwa ni Fool lakini nchini inakwenda kwa kuwa kuna watu wanamsaidia wapo chini yake.

Fuatilia hii Link umsikilize:-

 https://youtu.be/NAgd--3gjfY

TAFSIRI YAKE NI NINI NA JIBU LAKE LINA SOMO GANI KWA VIONGOZI?

#Kuna msemo wa Kiswahili usemao "Nionyeshe marafiki zako nijue tabia zako" ikiwa na maana kwamba wanaokuzunguka wana mchango mkubwa sana kukufanya ulivyo. Kama ukikaa na wenye tabia ya kukata tamaa na wewe utakuwa unakata tamaa kwenye mambo yako, ukikaa na wanaofikiria chini ya kiwango na wewe utakuwa unafikiria chini ya kiwango.

#Angalia uhusiano uliokuwepo kati ya Socrates na Plato. Plato alikuja kuwa alivyo kutokana na ukaribu wake na Socrates kwa hiyo Plato ni zao la Socrates na Aristotle ni Zao la plato. Amini wanaokuzunguka wanakufanya ulivyo. Kama Plato angelizungukwa na Mvua Samaki na yeye angelikuwa mvua Samaki. Angezungukwa na wacheza kamari na yeye angelikuwa mcheza kamari.

#Nani anamjua rafiki yake mkubwa Karl Max alikuwa nan? Kamsome mtu anayeitwa Fredrick Angels, Japokuwa walikuwa wanaishi mbalimbali ila mawazo yao ya kijamaa hayajawahi kutofautiana kwa kuwa hawa walikuwa marafiki.

#Kwa hiyo kama kila Kiongozi atafanya tathimini ya watu wanaomzunguka na kuwaondoa wale wote ambao sio Smart atapata mabadiliko makubwa sana katika uongozi wake.

#Angalieni baadhi ya wabunge wetu wamezungukwa na kina nani, wakuu wetu wa mikoa wamezungukwa na kina nani, mawaziri wetu wamezungukwa na kina nani, wakuu wa wilaya wamezumgukwa na kina nani halafu chunguza wanayoyawaza na wanayoyafanya yatakuwa yanalingana uwezo na waliomzunguka.

#Hata kama kiongozi ana akili kubwa kiasi gani kama wanaomzunguka watakuwa wajinga hatoweza kufanya kitu cha maana. Unayoyafanya yanalingana na aliyekuzunguka (Rafiki yako au msaidizi wako).

#Kumeibuka katabia flan hivi Afrika kwa viongozi kuchukia watu wenye uwezo. Badala ya kukaa nao karibu wanatafuta namna ya kuua Talent zao kabisa. Wanaogopa watawaoutshine watu wanaibuka na idea badala ya kusikilizwa wanaachwa na Kupuuzwa.

#Kwa Mataifa mengi ya Africa swala la uwezo linapuuzwa sana waliopo madarakani wanajifungia na wanajiona wao wanaweza kuliko wengine na ndio maana mataifa yetu hayaendelei.

#Marekani ipo ilipo kutokana na Kuheshimu tallent. Yaani majasusi ya Kimarekani yakitambua una akili kubwa watakufwatilia na hata kukushawishi upate uraia wa Marekani na sio kukufungia au kukupoteza.

#Marekani ipo ilivyo kutokana na kuheshimu akili za wajewish waliopo marekani. Ndio taifa la Pili duniani lenye wajewish wengi zaidi duniani ukiiacha Israel ambayo ndio asili yao. Ndio hawa wanaosafiri kwenda kwenye sayari nyingine kama wanaeenda Sokoni.

#Kagame mwaka 2013 alimpa uwaziri mtanzania Prof Lwandama kutokana na uwezo wake wa kiakili ndio huyo anayejenga Miundombinu ya Rwanda. Mifano ni mingi sana.....

Cha msingi cha Kujifunza tuheshimu Akili na Talent za watu pia kwa viongozi wetu wafanye Screening upya ya wanaowazunguka waone mabadiliko makubwa watakayoyapata.

Ole Mushi
0712702602