SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Jumamosi, 19 Agosti 2017

T media news

Makamu Wa Rais Ahudhuria Mkutano Wa Troika Mbili Mjini Pretoria,nchini Afrika Kusini

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassana , jana tarehe 18 Agosti 2017 amehudhuria Mkutano wa Troika Mbili za Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika SADC na Troika ya SADC kwa ajili ya kujadili hali ya Siasa , Ulinzi na Usalama katika Kanda.

Mkutano huu umejadili zaidi hali ya Siasa nchini Lesotho na namna ya kuisaidia Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ambayo inatarajiwa kufanya Uchaguzi Mkuu.

Taarifa kamili ya Mkutano huu itawasilishwa kesho Jumamosi tarehe 19 Agosti 2017, katika Mkutano wa 37 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika SADC.

Double Troika inahusisha nchi wanachama Sita ambao kwa sasa ni Swaziland, Tanzania, Afrika Kusini, Angola, Botswana na Msumbiji.

Imetolewa na

Ofisi ya Makamu wa Rais

Pretoria, Afrika Kusini

18 Agosti, 2017.