Ndege mbili ndogo aina ya aina ya Cessnas kutoka shule moja ya ufunzi wa urubani zimegongana huko Canada, katika anga ya eneo la shughuli za kibiashara na kuanguka. Mtu mmoja amefariki na wengine watatu wamejeruhiwa vibaya katika ajali hiyo.
Polisi walisema kuwa ndege hizo kila moja ilikuwa na rubani mmoja.
Ndege moja ilianguka katika egesho la magari, na nyingine ikaanguka juu ya paa la mojawapo ya maduka makubwa ya eneo hilo nje kidogo mwa mji wa Montreal.
Mashahidi walisema kuwa walisikia kishindo kikubwa na mtu mmoja akapiga kelele kuwa watoke nje ndipo walipoona ndege iliyokuwa imeharibika kabisa.

