Gianni Infantino baada ya kuingia madarakani, aliongeza wigo wa wajumbe wa baraza kuu la FIFA, mwanzoni lilikuwa na wajumbe 24lakini ameongeza hadi kufikia wajumbe 36.
Kwa hiyo Afrika na yenyewe imeongezewa idadi ya wajumbe wa kuingia kwenye baraza kuu la FIFA, nafasi hizo za wajumbe wa baraza kuu kwa upande wa Afrika zimegawanywa kwa zones. Kuna mwakilishi kutoka nchi zinazozungumza lugha ya Kifaransa (Francophone countries) sambamba na mwakilishi kutoka nchi zile zinazozungumza English (Anglophone countries).
Tenga (Tanzania) na Kwesi Nyantakyi (Ghana) ambaye ni rais wa chama cha soka cha nchi hiyo ndio wanagombea nafasi moja, kesho watakuwa wanapigiwa kura ili kumpata mjumbe mmoja atakaeingia kwenye baraza kuu la wajumbe wa FIFA.
Iwapo Tenga atafanikiwa kupigiwa kura nyingi, ataingia kwenye baraza kuu la FIFA na itakuwa ni faida kwa Tanzania.
Wajumbe hao watakaochaguliwa, wataungana na wajumbe wengine kukamilisha idadi ya wajumbe 36 wa baraza kuu la FIFA ambapo watakutana kwa mara ya kwanza kati ya October 13 na 14 huko Zurich, Uswis.
