sarakasi za Mgogoro wa kisiasa nchini Gambia,zinazidi kuchukua hatua nyingine kila uchao,kufuatia Umoja wa Afrika,AU,kuunga mkono suluhu ya sakata hilo kufikiwa kwa amani na mahakama ya nchi hiyo.
Tayari mahakama ya kikatiba ya Gambia, imeshaanza kushughulikia kadhia hiyo kufutia Rais Yaya Jameh,kufungua kesi kupinga matokeo ya Uchaguzi wa Rais wa nchi hiyo kwa madai kadhaa ikiwemo udanganyifu.
Kwa mujibu wa vyombo vya habari wananchi wa Gambia,wamedai kuwa hiyo ni dalili njema kupatikana suluhu ya mzozo huo wa kisiasa kwa amani.
Viongozi wa AU,walioko nchini humo,mbali na kumtaka bwana Yaya Jameh,kuheshimu matokeo ya Uchaguzi,wamesema,ni vyema mzozo huo ukatatuliwa kwa njia ya amani na kugeuka matamshi yake ya awali ya kumtaka Rais Yaya Jameh,kuheshimu matokeo yaliyotangazwa na tume ya Uchaguzi na kukabidhi madaraka kwa amani.
Hata hivyo wakosaji wake,wanadai kuwa hatua hiyo ya Bwana Jameh,ni janja yake ya kubaki madarakani kwakuwa ana ushawishi mkubwa katika chombo hicho cha haki.