Bondia Francis Cheka akitoka nje ya ukumbi wa Mango Garden baada ya kugoma kupima uzito
Bondia Abdallah Pazi "Dula Mbabe" akipima uzito kwa ajili ya kupambana na Francis Cheka hapo kesho katika ukumbi wa Mango Garden jijini Dar es salaam leo
Mdogo wake Francis Cheka, Cosmas Cheka, akiongea a baadhi ya wadau wa ngumi juu ya swala la Kaka yake kutopewa pesa ya kianzio kabla ya kupima uzito
Mashabikiwa mchezo wa ngumi wakiwasili katika ukumbi wa Mango Garden Kinondoni kushuhudia jinsi mabondia hao wanavyopima uzito
Baadhi ya wadau wakijaribu kuzungumza na Cheka baada ya kugoma kupima uzito mpaka atakapopewa pesa yake
Bondia wa mchezo wa ngumi za Kulipwa nchini,Francis Cheka amegoma kupima uzito kwa ajili ya pambano lake dhidi ya Dula Mbabe mpaka hapo atakapopewa shilingi 3000,000/- kama kianzio kabla ya kupanda ulingoni.
Cheka amegoma kupima uzito katika ukumbi wa Mango Garden ambapo mpinzani wake tayari alikuwa ameshawasili tayari kwa ajili ya kupima.
“Nimetoka Morogoro kwa nauli yangu na nimelala hoteli kwa fedha yangu na nimejaribu kumpigia promota wangu Kaike mara kdhaa toka jana hakupokea simu. Nilivyofika hapa nikamuomba anipatiea fedha yangu bado akagoma. Hivyo mimi nimeamua kutopima uzito wala kucheza mpaka hapo nitakapopewa fedha yangu”amesema Cheka.
Baada ya kushindwa kuelewana bondia Francis Cheka aliamua kuondoka ukumbini hapo na kurudi hotelini alipofikia kujiandaa na safari ya kurejea Morogoro kuendelea na mambo mengine.
Kwa upande wake promota wa mchezo huo Siraju Kaike alisistiza kuwa pambano hilo lipo licha ya bondia huyo kugoma kupima uzito kutokana na kutokubaliana katika masuala ya kifedha. Hakufafanua.