Wakati mgumu unaupitia hata kama una pesa nyingi au kidogo. Haya ndiyo yanamtokea mchezaji wa Ivory Coast Emmanuel Eboue ambaye kwa sasa anapitia kipidi kigumu baada ya kufungiwa kucheza soka kwa muda wa mwaka mmoja.
Eboue amefungiwa baada ya kukataa kumlipa wakala wake ambae alifikisha kesi kwenye mamlaka husika. Baada ya hapo sheria ilichukua mkondo wake na Eboue alifungiwa kwa muda wa mwaka mmoja ambapo anatarajiwa kurudi uwanjani ikifika mwezi wa tatu.
Akiongea na gazeti la Telegraph Eboue amezungumzia upweke wake na kutengwa na marafiki zake wa karibu kiasi cha kufikia hatua za kufikiria kwamba hakutana tena kuamka kitandani.
“Inafika siku ambayo sikuhitaji tena kuamka kitandani. Siku moja nilitaka kujiua lakini familia yangu inanifanya nijiskie mwenye nguvu. Wao peke yao nawafikilia niwapa mpweke. Nawaza sijui ningekuaje kama nisingekua nao”.
Eboue pia alimtupia lawama mshkaji wake wa kitambo Kolo Toure,“Wakati Kolo alivyokuwa amefungiwa nilikua naongea na yeye kwenye simu mara nyingi. Najua alikua na wakat mgumu na huo ndio rafiki wa kweli anaonekana. Sitaweza kusema vibaya kuhusu yeye kwasababu bado namuona ni kaka yangu. Natumaini siku moja atanipigia simu lakini hiki kinachotokea kinanivunja moyo sana. Nilidhani urafiki wetu ulikua mkubwa sana.”