Imetokea Brazil na Mwanamke mwenyewe anaitwa Vera Lucia da Silva na umri wake ni miaka 44 ambapo aliamua kukaa kwenye jeneza siku nzima ili apate uzoefu wa mazingira ya kifo ili siku akifa asiwe mgeni na Jeneza.
Vera aliamua kukaa kwenye jeneza huku familia yake ikifanya vitu vinayofanywa kwenye msiba ili aone inakuaje ambapo baada ya kutoka humo alisema ilikua siku nzuri zaidi kwenye maisha yake yote.
Sherehe hiyo ya kujifunza maisha ya kwenye Jeneza ambayo ilifanyika Jumatano ya November 2 2016 ni sherehe ambayo ilifanyika kwenye eneo la makaburi.