SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Jumatano, 17 Agosti 2016

T media news

MWANARIADHA MTANZANIA ATAJA VIONGOZI WALIOMWANGUSHA OLYMPIC 2016

Mashindano ya Olympic 2016 yanazidi kushika kasi hapa katika mji wa Rio nchi Brazil huku washiriki wa kutoka Tanzania wakiwa wameshindwa kufanya vizuri kwa mara nyingine tena katika mashindano haya makubwa ambayo hufanyika kila baada ya miaka minne (4).

Nimekutana na mwanariadha Sara Ramadhani kutoka Tanzania ambaye alishiriki mbio za marathon kilometa 42 na kumaliza mashindano akiwa katika nafasi ya 121, nimefanya naye mahojiano mafupi nikitaka kujua kwanini ameshindwa kufanya vizuri kwenye mashindano haya na atarejea nyumbani Tanzania akiwa mikono mitupu.

shaffidauda.co.tzHongera sana Sara kwa kumaliza mbio za kilometa 42, watanzania wangependa kujua ni kwanini mshiriki wao hakufanya vizuri kwenye mashindano haya?

Sara: Nashukuru nimemaliza salama lakini nimepata matatizo mengi, sikuwa na mtu wa kunipa maji kwenye vituo kwasababu wote walikuwa ndani hata daktari pia alikuwa ndani hawajui mchezaji anaendeleaje ni vitu vingi ambavyo nilistahili kufanyiwa lakini sikufanyiwa.

shaffidauda.co.tzUnadhani maandalizi mengine yalikuwa vizuri kabla ya mashindano?

Kabla ya mashindano nilikuwa nafanya mazoezi vizuri nilkuwa na kocha wangu Francis ambaye nadhani anaingia Rio leo tulikuwa kambi ya Moshi, Kilimanjaro West nilifanya vizuri na nilitegemea kufanya vizuri lakini mambo kama haya yaliyotokea, hakuna kiongozi hata mmoja aliyeenda kwenye kituo. Wachezaji wengine wanapata maji lakini mimi sina mtu wa kunipa maji.

Sara: Hata daktari hakuja kunifatilia labda pengine naweza kupata matatizo huko lakini yeye alikuwa amekaa ndani.

shaffidauda.co.tzKabla ya amashindano kuanza ulikuwa na matarajio gani?

Sara: Kabla ya mbio kuanza nilikuwa naomba Mungu niwepo kwenye nafasi ya zawadi lakini yametokea matokeo kama hayo.

shaffidauda.co.tzHii ni mara ya ngapi unashiriki mashindano ya Olympic?

Sara: Ni mara ya kwanza.

shaffidauda.co.tzWanamichezo wa Tanzania wamekuwa hawafanyi vizuri kwenye mashindano haya ya Olympic. Riadha ndiyo mchezo ambao ulikuwa unafanya vizuri na kuipeperusha vyema bendera ya Tanzania pamoja na ngumi, unadhani sikuizi tatizo ni nini kwasababu watanzania kila wanapokwenda kushiriki mashindano haya wanarudi mikono mitupu

Sara: Inategemea maandalizi na viongozi jinsi walivyojipanga. Unakuta mnapewa pesa nusu, mnaambiwa mkirudi mtamaliziwa pesa iliyobaki lakini nchi nyingine kama Kenya, Uganda, Ethiopia na wengine wanakabidhiwa pesa zao palepale. Sasa sisi tutakuwa na matumaini na moyo gani wa kujituma? Tanzania bado tuko nyuma.

shaffidauda.co.tzOlympic ya 2020 Tokyo, Japan utakwenda kushiriki?

Sara: Mungu akinijalia uzima, nitakwenda.