Mwanamitindo na msanii wa muziki Jokate Mwegelo amemkazia msanii Q Chief na kuhitaji pesa nyingi ili yeye aweze kushiriki kama video queen katika video mpya ya Q Chief ambayo inatarajiwa kutoka siku za usoni.
Q Chief anasema kuwa anavutiwa sana na msanii huyo kiasi cha yeye kumuimba kwenye wimbo wake mpya na alitamani sana angeweza kuwepo kwenye video hiyo lakini anadai alipomfuata alimtajia pesa nyingi kiasi cha Q Chief na uongozi wake kushindwa.
"Jokate ni mzuri, ana mvuto na kila mtu anampenda yeye, ilikuwa yeye awe 'video queen' kwenye wimbo wangu mpya lakini kwa bahati mbaya Jokate kataja pesa nyingi sana. Nilivyomfuata alinipokea vizuri kwani ana heshima na maadili na sikutegemea jinsi alivyonipokea unajua tena yule shemeji yetu. Lakini kibiashara sasa tuliwasikiliza na kuwaelewa ingawa na sisi tulifikiria tukaona kiwango kile ni kikubwa sana" Alisema Q Chief
Mbali na hilo Q Chief alisema yeye anaheshimu kazi ya Jokate na kudai kuwa ni moja ya wanawake ambao hata akikaa sura yake inamjia tu hata kama hayupo naye kwenye mahusiano