Habari zilizoenea kwenye mitao ya kijamii ni kwamba Mwenyekiti wa Yanga Yusuf Manji ameamua kujiuzulu wadhifa wa uenyekiti katika klabu hiyo pamoja na kusitisha zoezi la kutaka kuikodi timu hiyo kwa miaka 10
kama ilivyokuwa dhamira yake hapo awali.
Kwa mujibu wa vyanzo vya ndani ya Yanga, inadaiwa kuwa bosi huyo ameamua kukaa pembeni ikiwa ni baada ya kuibu kwa mijadala mikubwa na baadhid ya watu kupinga uamuzi wake wa kutaka kuikodi Yanga.
“Natukanwa sana na baadhi ya matajiri ambao ni wapenzi wa Yanga…hawapendi mimi niwepo pale. Pesa ni yangu natoa kwa mapenzi niliyonayo kwa klabu yangu…kwanini nitukanwe wakati sipati maslahi yoyote? Najiuzulu,” Ni kauli ya mwenyekiti wa Yanga SC ambaye ametangaza kujiuzulu kufuatia kusakamwa na hasa baada ya kuomba kuichukua Yanga kwa miaka 10. (kwa mujibu wa facebook page ya Naipenda Yanga).
Hata hivyo kumekuwa na vikao mbalimbali kumsihi Manji abadili maamuzi yake lakini inaonekana amechoka na ameamua kuibwaga Yanga. Tayari Reginald Mengi ameonesha nia ya kuingia Yanga endapo Manji ataondoka. Leo jioni baraza la wazee linataraji kuwa na kikao na Mengi.