SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Alhamisi, 8 Juni 2017

T media news

HABARI NA HISTORIA YA KABILA LA WADIGO.



Wadigo ni moja ya kabila linalopatikana nchini Tanzania. Ukiwa nchini Tanzania kabila hili la Wadigo linapatikana katika mkoa wa Tanga. Kabila la wadigo ni moja ya kabila lenye kuthamini na kutunza sana tamaduni zao.  Kabila hili ni la kibantu waliopata kufika maeneo ya Udigo hata kabla ya miaka 500. Na hata kwenye miaka ya 900-1000 kipindi ambacho wageni kutoka mashariki ya mbali walikuta Wenyeji wa maeneo ya pwani wakiwa na wahusiano ya kibiahsra na wadigo. Kwa nama  hiyo wadigo walikuwa moja ya sehemu ya biashara ya wakati huo.

 Haikuishi hapo hata kwenye miaka ya 1800, kipndi cha kuanzishwa kwa ukoloni barani afrika. Wadigo ni moja ya watu waliofikiwa na wageni hao ambao ndio wakoloni.
Na wakati wakoloni wanaingia maeneo ya Wadigo, walikuta Wadigo wakiwa na maisha yao na uongozi wao. Na hata wakiwa wanaandika habari za watu wa maeneo hayo, waliwatambua kama Wadigo.

ukweli ni kwamba kabila hili la Wadigo lina histroia kubwa sana.lakinin kwa kuwa mkoa wa Tanga kuna makabila mengi ambayo yametoka katika kabila moja ambalo ni Wazigua. hivyo asilimia kubwa historia ya Wadigo ilimezwa na Wazigua kwa upande flani hivi. Kwani tunapozungumzia mkoa wa Tanga tunazungumzia Wazigua ambao waligawanyika katika makundi yake yasiopunga matano yaani Wazigua wenyewe, Wasambaa, Waluvu na Wabondei

Kwa mujibu wa masimulizi ya Wazee na baadhi ya wataalamu kama wakina Nkondokaya na Kayamba wanasema kuwa, Wadigo wanatokea hama wanaishi nchini Tanzania na waengine wanaishi nchini Kenya hasa maeneo ya  Magodi na Shungwaya. Na waliahama huko na kuja Tanzania kutokana vita vilivyowahi kutokea kwenye miaka ya 1700. Vita hivyo vilikuwa vinahusisha koo mbalimbali za Wagala na makabila mengine ya huko Kenya hasa hasa kabila la Wakamba na bila kusahau vita vya Waturukana na Wanandi.

Asili ya kabila hili la Wadigo  linazua  mijadala mingi sana. Mijadala hiyo inazuka kwa kuwa kumetokea masimulizi mengi juu ya asili ya jina Wadigo. Lakini tukirejerea maandiko ya Nkondokaya na masimulizi ya wazee mbalimbali kutoka Tanga, wanasimulia kuwa; neno Wadigo linatokana na jina la mtu mmoja  aliyefahamika kwa jiana la Digo au Dibwa. Na inasimuliwa kuwa mtu huyo alikuwa maaraufu sana na hata siku ailyokufa, watu waliamua kupaita eneo hilo kwa Mdigo. Na hivyo wageni na watu wengine waliwatambua watu wa maeneo hayo kuwa ni Wadigo wakimaanisha kwa Yule mtu maarufu. Hivyo jina hilo likakua na kuenea na hata watu hao walijitambulisha kwa jina hilo.

 Hivyo  miaka ya baadae kukatambulika kwa jina la Wadigo ikimaanisha kuwa watu wanaopatikana eneo la kwa mzee Digo. Na kwa kuwa watu hao walikuwa wanaish pamoja na mila ma desturi zao zinafanana wakaamua kuitwa Wadigo. Na hata wageni waliofika hapo waliandika hivyo na hata wazee husimulia hivyo kwa watoto wao.