Mara nyingi kumekuwa na tabia ya kuthamini zaidi washambuliaji na makocha endapo inatokea timu imeshinda na kusahau magoli hayo yametokana na muunganiko wa nguvu ya wachezaji wote.
Mabeki na viungo hufanya kazi kubwa na kupelekea washambuliaji kupata rahisi tu ya kuukwamisha mpira wavuni huku lango lao likibaki salama.
Sasa leo tunaangazia kundi la wachezaji ambalo limeshahaulika, kundi ambalo linatoa mchango mkubwa sana kuwalinda mabeki na makipa. Hili ni kundi la viungo wakabaji. Huwa wana kazi kubwa sana…wanapiga tackles, interceptions, kublock mipira na mengine mengi.
Hivyo basi hapa tunawaangazia viungo wakabaji bora sita ambalo walikuwa nyota msimu uliopita wa Ligi ya England.
Cheikhou Kouyaté – West Ham
West Ham ilikuwa ni timu imara sana msimu uliopita. Kati ya michezo 31 ya EPL aliyocheza, Msenegali huyu alifunga mabao matano na kutoa pasi mbili za magoli. Aliisaidia timu yake kuifunga miamba ya Manchester City, Chelsea, Liverpool na Arsenal. Alifanya kazi kubwa sana ya kusaidia kuounguza kasi ya mashambulizi pamoja na kusukuma mashambulizi mbele.
Akiwa bado amebaki klabuni hapo kuelekea msimu ujao, Cheikhou Kouyaté atakuwa ni msaada mkubwa kwa kocha wake Slaven Bilic.
Victor Wanyama – Southampton
Mkenya huyu ni moja ya viungo hoadari kwa sasa nchini England. Anasafisha hatari zote zinazonusa langoni mwao na kuwalinda mabeki wake Fonte na Yoshinda. Alifanya kazi kubwa msimu uliopita na kuisaidia timu yake ya Southampton kupata nafasi ya kushiriki Michuano ya Europa msimu ujao. Tayari ameondoka Southampton baada ya kusajiliwa na Tottenham Hotspurs katika usajili wa majira haya ya kiangazi.
Francis Coquelin – Arsenal
Francis Coquelin alifanya mapinduzi makubwa katika safu ya kiungo ya timu ya Arsenal. Alikuwa akianua uchafu wote uliokuwa ukizengea langoni mwao. Alikuwa hodari sana kwa kupiga tackling, interceptions, na kuwania mipira ya juu (aerial duels). Alipata nafasi hiyo baada ya aliyekuwa nahodha wa timu hiyo Mikel Arteta na mkongwe Mathieu Flamini kupata majeraha. Alitoa msaada mkubwa kwa timu hiyo msimu uliopita.
Eric Dier – Tottenham Hotspurs
Huyu alifanya kila kilichotakiwa kufanywa na kiungo mkabaji yeyote yule ambaye anatimiza majukumu yake. Alikuwa bora sana msimu uliopita kwa upande wa Spurs chini ya kocha wao kijana Mauricio Pochettino.
Fernandinho – Manchester City
Watu wengi watashangaa kwanini Fernandinho badala ya Yaya Toure, lakini kama ulikuwa ukiangalia kwa uzuri michezo ya Manchester City msimu uliopita, Fernandinho alikuwa akicheza nyuma na Toure na ama hakika alifanya kazi zote za kuondoa hatari zisiwafikie mabeki wake wa kati pamoja na kipa wake.
Ng’olo Kante – Leicester City
Unapozungumzia mafanaikio ya Leicester City mpaka kuchukua ubingwa msimu uliopita, basi huwezi kuacha kumzungumzia kiungo Ng’olo Kante. Alikuwa akifanya kazi zote chafu pamoja na kusaidia kusukuma mashambulizi kwa wapinzani. Riyad Mahrez na Jamie Vardy wote walipata ssifa kubwa sana lakini beki Wes Morgan, Robert Huth pamoja na kipa Kasper Schmeichel ndio wanajua Ng’olo Kante alikuwa akifanya nini kwenye timu.
Tayari ameshasajiliwa na Chelsea kuelekea msimu mpya wa ligi.