Uwazi Showbiz
STAA wa Muziki wa Bongo Fleva, Mwanaisha Said ‘Dayna Nyange’ amemfungukia staa wa Hip Hop Bongo, Billnas kuwa hakuna uhusiano wowote wa kimapenzi unaoendelea kati yao zaidi ya kazi ya kimuziki.
Akichonga na Uwazi Showbiz, Dayna anayebamba na Ngoma ya Komela alisema kuwa awali hakuwa akimjua Billnas lakini baada ya kumuona kwa mara ya kwanza kipindi cha nyuma katika Studio za Free Nation kwa Prodyuza T. Touch ndipo walipoanza kujuana.
“Siku moja nilimpigia simu, alikuwa Sauz (Afrika Kusini) kwa shughuli zake za kisanii, nikamwambia nahitaji kufanya ngoma naye. Alikubali na kuanzia hapo tukawa karibu ila kikazi tu, yeye ana uhusiano wake na mimi kivyangu,” alisema Dayna.