SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Jumapili, 24 Julai 2016

T media news

MLIPUKO WAUA WATU 80 AFGANISTAN



 
 


 
 
 

Wizara ya afya nchini Afghanistan imesema takibani watu 80 wameuawa na zaidi ya wengine 150 kujeruhiwa katika shambulio la kujitoa mhanga lililofanyika kwenye Mji Mkuu Kabul.

Baadhi ya taarifa zinasema kulikuwa na milipuko miwili.

Shambulio hilo linaonyesha kuwa lililenga maandamano ya maelfu ya watu kutoka jamii ndogo ya Hazara, ambao hujikuta wakidhalilishwa na kufanyiwa ukatili.

Walikuwa wakiandamana kupinga mpango wa serikali wa kuhamisha umeme kutoka kwenye majimbo yao katikati ya nchi.