Wasanii wa muziki Jux pamoja na Mrisho Mpoto kila mmoja kwa wakati wake ameamua kuwa mfano kwa Watanzania kwa kutembelea vivutio vya utalii.
Jux ambaye kwa sasa anafanya poa na wimbo ‘Wivu’ aliambatana na mpenzi wake Vanessa Mdee kutembelea katika mbuga ya wanyama ya Serengeti iliyopo mkoani Arusha.
Kupitia instagram, Jux alipost picha ya Vanessa na kuandika:
Day 1 at #SasakwaLodge was nice but the Queen arrived on Day 2 so we had to upgrade for that better view #FaruFaru is almost as dreamy as her #Tanzania #Serengeti #Vacation
Kwa upande wa msanii wa muziki wa asili Mrisho Mpoto, alifanikiwa kuupanda mlima Kilimanjaro.
Kupitia instagram, Mpoto aliandika:
Haikua kazi rahisi, kila anaeomba anapaswa kushukuru. Nawashukuru wote mlionieombea nna mengi sana sana ya kuhadithia.Everyone who asks for Prayers must be thankful too. I Thank you so much for your prayers and good wishes. It has never been easy! I have got a lot to share with you guys.
Angalia picha mbalimbali za mastaa hao.