SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Jumatano, 29 Juni 2016

T media news

MAONI YA MDAU: BURE YA MANJI ILIVYOIATHIRI YANGA

Na Isack, Babati Manyara

Kitengo walichofanya Yanga cha kuruhusu mashabiki kuingia bure uwanjani kwenye mchezo kati ya Yanga dhidi ya TP Mazembe kimeikosesha klabu fedha nyingi sana ambazo wanazihitaji kwa kuendekeza siasa ambazo hazina maana.

Kulikuwa hakuna sababu ya kuacha mashabiki waingie uwanjani bure lakini kwa sababu ya siasa za soka la kibongo, waliona sawa kukubali kuingia hasara. Mechi kubwa dhidi ya TP Mazembe walitakiwa waitumie vizuri kupata pesa ambayo wangewalipa posho nzuri wachezaji wao na hata kufanya usajili wa wachezaji wapya.

Katika hili TFF pia wameonesha udhaifu, wameshindwa kuwazuia Yanga kuruhusu mashabiki kuingia bure kitu ambacho ni hatari kiusalama hususan katika mechi ya kimataifa ambayo inasimamiwa na CAF.

Vurugu zilitotokea uwanjani wakati watu wakijaribu kulazimisha kuingia uwanjani baada ya mageti kufungwa ni baadhi ya matukio ambayo yalihatarisha usalama, kuna mageti yalivunjwa, huku kukiwa na uharibifu mwingine kama mabomba ya gesi haikuwa kitu chema.

Kama vurugu zile zitaonekana CAF basi tutarajie matamko mazito kutoka CAF, lakini nilipongeze jeshi la polisi kwa uhodari wao wa kuwadhibiti mashabiki waliokuwa nje wakilazisha kuingia ndani. Najiuliza kama ingetokea jeshi la poli lingezidiwa nguvu na mashabi halafu ile halaiki iliyofurika pale nje ya uwanja wa taifa sijui hali ingekuwaje.

Nina hoja zangu 9 ambazo ninataka nizifikishe mbele ya uongozi wa Yanga na watanzania kwa ujumla baada ya kuwatangazia mashabiki wataingia bure kwenye mchezo huo;

Timu yetu ya Yanga imetangaza kiingilio bure na wakati timu inamtengemea Manji peke yake, fedha za viingilio zingepatikina mfano 200m zingeweza kulipa mishahara ya wachezaji hata kwa miezi miwili au zaidi.Fedha hizo zingeweza kurekebisha uwanja wa Kaunda na timu ingeweza kufanyia mazoezi hapo na kupunguza gharama za kukodi viwanja.Fedha hizo zingeweza kusajili wachezaji wa ndani zaidi ya 5 @ 30 na kuwalipa mishahara msimu mzima.Salumu Telela ameondoka ni mchezaji muhimu sana ndani ya Yanga angeweza kulipwa pesa ya usajili na kuendelea kukipiga Jangwani, bado uwezo wake ni mkubwa sana.Kama Yanga ni tajiri kiasi kwamba haioni haja ya kuchukua viingilio, kwa nini haina uwanja hata wa mazoezi mpaka fedha nyingi kiasi hicho zinapotea?Katika maisha yangu yote miaka (29) sijawahi kusikia Man United, Barca wala timu nyingine ikifanya mambo ya ajabu kama haya ilihali zinauwezo wa kutosha, au viongozi wetu wanamatatizo gani mpaka wanaruhusu watu kuingia bure?Kama Yanga wanauwezo kwa nini waliipigia kelele TFF kuhusu Azam TV kuwa itashusha mapato kutokana na mechi yao kuoneshwa kwenye TV?Kama huu ulikuwa ni ushauri wa Jerry, basi anamshauri vibaya Manji, leo hii Manji akitoka tu Yanga hakuna mtu anayeweza kulipa mishahara wachezaji hata kwa mwezi mmoja na Jerry atakimbia na Yanga itabaki yatima.Sisi tunataka club ijitegemee huku fedha zinapotea bure au kuna mganga aliwaambia mashabiki wakiingia bure uwanjani Yanga itaifunga TP Mazembe?

Mwisho nashauri viongozi wa Yanga waache kulumbana na TFF wala CAF bali washirikiane na TFF, malumbano hayajengi.

0715163816