Fainali ya UEFA Champions League ndiyo inasubiriwa kwa hamu kubwa na mashabiki wa soka ulimwenguni kote ambapo miamba ya soka la Hispania itakuwa ikiwania taji hilo maarufu kwenye kwa ngazi ya vilabu barani Ulaya.
Baada ya kuonesha ubora na performances ya hali ya juu kwa miezi 9 iliyopita, Atlètico Madrid na Real Madrid zitakuwa zikichuana Jumamosi kutafuta mshindi mmoja wa taji la vilabu bingwa Ulaya ndani ya uwanja wa San Siro mjini Milan.
Ikiwa ni marudio ya fainali ya mwaka 2014, ambayo ilisubiri dakika 120 kuamua timu gani itasinda ubingwa, msimu huu umebeba historia tofauti huku wapinzani hao wa soka la Hispania wakiwa kwenye form ya hatari.
Hapa tunaangalia njia zilizopita timu hizi hadi kufika hatua ya fainali…
Road to the final: Real Madrid
Real Madrid wamefanikiwa kufika Milan kwenye fainali ya Champions League wakitokea kundi A ambalo liliundwa na timu za PSG, Shakhtar Donetsk na Malmo FF. Real Madrid walimaliza hatua ya makundi wakiwa vinara wa kundi lao kwa pointi zao 16 baada ya kucheza michezo 6.
Katika mechi 6, Madrid ilishinda mechi 5 na kutoka sare mchezo mmoja huku ikiwa haijapoteza pointi hata moja.
Ilikuwa ni vigumu kuizuia Madrid isipate ushindi ndiyomaana ikashinda mechi 5 kati ya 6 kwenye hatua ya makundi. Ushindi mkubwa wa Madrid ulikuwa ni wa magoli 8-0 dhidi ya Malmo ambao walifungwa tena 2-0 kwenye mchezo wa marudiano kwenye uwanja wao nyumbani. Wababe hao wa Hispania wakaishinda Shakhtar 4-0 nyumbani kisha 4-3 ugenini kabla ya kuichapa 1-0 PSG nyumbani na kutoka sare ya 0-0 kwenye mchezo wa marudiano mjini Paris.
Madrid ilifunga jumla ya magoli 19 na kuruhusu kufungwa magoli matatu pekee na kufanya tofauti ya magoli ya kufunga na kufungwa kuwa 16.
Madrid imezitoa Roma, Wolfsburg na Manchester City kwenye hatua ya mtoano
Real Madrid tayari imeshashinda mara moja Italy kwenye michuano ya Champions League msimu huu, ushindi huo ulikuja kwenye hatua ya 16 bora dhidi ya AS Roma.
Vujana wa Zinedine Zidane walikuwa kwenye kiwango kizuri kwenye mechi zote mbili wakitoa kichapo cha magoli 2-0 mjini Roma na kushinda tena ushindi wa magoli 2-0 kwenye uwanja wa Bernabeu.
Mchezo pekee ambao walilala ulikuwa ni ule wa kwanza wa hatua ya robo fainali walipokubali kipigo cha magoli 2-0 lakini wakarejea kwenye reli na kupata ushindi wa magoli 3-0 kwenye usiku wa kukumbukwa pale Bernabeu.
Wapinzani wa hivi karibuni wa Real Madrid walikuwa ni Manchester City kwenye hatua ya nusu fainali ambapo kikosi cha Zidane kilichomoza na ushindi wa bao 1-0 na kujikatia tiketi ya kucheza fainali msimu huu baada ya mchezo wa awali kumalizika kwa sare ya bila kufungana.
Rekodi zinaonesha Real Madrid imepata ushindi kwenye michezo 9, sare mbili huku ikiwa imepoteza mchezo mmoja. Imefunga magoli 27 huku yenyewe ikiruhusu magoli matano, hakuna timu nyingine iliyoshinda mechi nyingi zaidi na yenye goal difference nzuri kama Real Madrid.
Safu ya ulinzi ya Real Madrid inaonekana kuwa ngumu kutokana na kucheza michzo takriban 10 kati ya 12 bila kuruhusu nyavu zao kutikiswa. Kikosi hicho kinatajwa kushinda mechi nyingi (9 kati ya 12) huku kikwa na wastani mzuri wa magoli ya kufunga na kufungwa (+22 goal difference).
Road to the final: Atlètico Madrid
Ni haki kusema kwamba ilipita kwenye njia yenye changamoto nyingi kuelekea mchezo wa fainali ya Champions League.
Atletico ilikuwa Kundi C pamoja na timu za Benfica, Galatasaray na Astana. Ilishinda michezo minne kati ya sita, ikatoka sare mara moja na kupoteza mchezo mmoja. Katika hatua ya makundi, ilifunga magoli 11 na kuruhusu nyavu zake kuguswa mara tatu na kufanikiwa kumaliza ikiwa na pointi 13 pointi tatu zaidi ya Benfica iliyomaliza katika nafasi ya pili kwenye Kundi C.
Atletico imezitoa PSV Eindhoven, FC Barcelona na Bayern Munich kwenye hatua ya mtoano
Kama ilivyokuwa kwa Real Madrid, Atletico ilimaliza katikia nafasi ya kwanza kwenye kundi lake kabla ya kupambana katika hatua ya 16 bora, ilibidi mikwaju ya penati iamua ni nani atasonga mbele kwenye hatua inayofuata hatimaye Madrid ikapenya kwa kiki za penati 8-7 mbele ya PSV Eindhoven na hapo vijana wa Diego Simeone wakawa kama wameonezewa nishati mpya kwani baada ya hapo walikuwa wakijiandaa kuwakabili mabingw watetezi FC Barcelona.
Pambano kati ya Barcelona dhidi ya Atletico lilikuwa na ladha ya aina yake katika michuano ya Champions League msimu huu, Barcelona walipata faida ya ushindi wa magoli 2-1 kwenye mechi ya nyumbani lakini Atletico ilizunduka na kufanya maajabu kwenye mechi ya marejeano pale Vicente Calderon.
Bao kutoka kwa Antoine Griezmann pamoja na mkwaju wa penati wa dakika ya 85 ulibadili mwelekeo wa matokeo ya mchezo wa kwanza na hapa mabingwa watetezi wa taji la UEFA Champions League wakalitema taji rasmi huku Atletico wakijitangaza wenyewe kwamba hawataki mchezo kwenye kinyang’anyiro cha taji hilo katika msimu huu.
Baada ya mchuano wa kukata na shoka dhidi ya Barcelona, wauaji hawa kutoka Hispania wakawekewa Bayern Munich mbele yao. Pambano jingine la kufa kiumbe likawa linawakabili wanaume wa Simeone, pambano hili liliamuliwa kwa faida ya goli la ugenini kutoka kwa Saul Niguez na Atletico ikaingia fainali kwa faida ya goli la ugenini baada ya matokeo ya jumla kusomeka 2-2 huku Atletico ikiwa ndiyo timu pekee iliyopata goli kwenye mechi ya ugenini.
Bayern Munich vs Atletico Madrid ililikuwa ni pambano la aina yake ambalo litabaki kuzungumzwa kwa miaka kadhaa ijayo.
Kwa mtazamo wangu, Atletico Madrid wamepita njia yenye changamoto nyingi hadi kufika hatua ya fainali, lakini vijana hawa wanastahili kuwa hapo walipo ukiangalia kiwango ambacho wamekuwa wanakionesha hasa kwenye mechi zenye presha kubwa.
Matazamo wangu
Kombe la UEFA linaweza kwenda upande wowote. Timu zote zimekuwa kwenye kiwango kizuri si kwenye michuano hii pekee, bali hata katika ligi yao ya Hispania (La Liga) ambapo timu zote ziliikimbiza FC Barcelona hadi mwisho kwenye kuwania taji la ligi ya nchini kwao.
Ikiwa ni klabu yenye mataji mengi ya Champions League (mataji 10), Real Madrid inauzoefu wa kushinda game ngumu za fainali ya ligi ya mabingwa Ulaya. Miongoni mwa game hizo ni ile fainali ya miaka miwili iliyopita, matokeo ya mechi ile yana uhalisia kidogo kwa mechi inayosubiriwa Jumamosi licha ya timu zote kuwa na ari mpya kwenye mchezo huo.
Hakuna ubishi mchezaji mwenye ushawishi mkubwa uwanjani atabaki kuwa Cristiano Ronaldo. Tayari ameshafunga mabao 16 akihitaji magoli mawili ili kuvunja rekodi yake mwenyewe ya magoli 17 aliyoiweka kwenye msimu wa 2013-14, mara zote star huyu wa Real Madrid amekuwa mwiba kwa upande wa safu ya ulinzi ya Atletico Madrid hata kama asipofunga goli.
Kwa upande wa Atletico Madrid, Antoine Griezmann amekuwa na mchango mkubwa kwenye timu. Akiwa na mabao 7 ambayo yameisaidia timu yake kufikia kwenye hatua ya fainali, atakuwa tegemeo kubwa kwenye mchezo wa fainali na huenda akaamua mchezo.
Speed, uwezo mkubwa wa kumiliki mpira pamoja na ubunifu wa hali ya juu, Saul Niguez ni mchezaji ambaye atatakiwa kuangaliwa kwa jicho la pekee na walinzi wa Real.
Akipambana kwenye michuano ya msimu huu, Fernando Torres anahitaji kunyanyua ndoo ya ubingwa wa Ulaya akiwa na Atletico. Licha kufunga goli moja kwenye mechi saba, Torres ni aina ya wachezaji wanaodhihirisha ubora wao kwenye mechi kubwa kama hii.
Eneo la ulinzi ndiyo silaha kubwa ya mafanikio ya Atletico kwenye michuano hii ya UEFA Champions League msimu wa 2015-16, na hii itatakiwa kudhihirika kwa mara nyingine tena siku ya Jumamosi.
Real Madrid inamiliki viungo washambuliaji hatari ambao wanaweza kuiweka timu pinzani kwenye presha kutokana na kumiliki mpira na uwezo wa kupiga pasi. Modric, Kroos na Bale ni aina ya wachezeshaji wenye uwezo wa kufunga pia licha ya kuwalazimisha mabeki kufanya makosa. Kuwaweka chini ya uangalizi viungo hawa itahitaji umakini wa hali ya juu ya wakabji wa Atletico Madrid.