Idara ya Baologia na Misitu SUA, imewashauri wananchi kuzingatia kanuni bora za kilimo cha miembe hasa kanuni za kuchagua aina bora ya upandaji wa miti hiyo kulingana na mahitaji ya soko.
Akizungumza na SUAMEDIA msimamizi wa wanafunzi wanaojifunza kwa vitendo bw. Mnyonge James amesema miti ya miembe inatakiwa ipandwe umbali wa mita 10 kwa 10 kama utatumia miembe ya kuunga, kwa sababu miti hii haiwi mikubwa sana na haiishi miaka mingi, kwa ile ambayo ya kuunga ipandwe umbali wa mita 15 kwa 15 kwa kila mti mmoja.
PICHA NA MTANDAO
Aidha Bwana Mnyonge amewataka wakulima kufanya ukaguzi wa mashamba mara kwa mara ili kudhibiti wadudu na magonjwa ya matunda kabla ya madhara hayajawa makubwa ili kupata mazao ambayo yatapata soko zuri na kuweza kuhifadhiwa muda mrefu.
Pia ameongeza kuwa unapopanda miti ya miembe unatakiwa kusafisha shamba ili kurahisisha uvunaji na wakati wa kuvuna hakikisha maembe hayadondoshwi chini ili kuepuka kuchubuka kwa matunda ama kupondeka hasa yale yaliyoiva .
Hata hivyo bwana Mnyonge amesisitiza kuwa miti inatakiwa ipandwe mita kumi na tano mpaka ishirini kutoka katika makazi ya watu, kwa sababu miti kama miembe huwa na mizizi mikubwa hivyo inaweza kubomoa nyumba.