Je, unafahamu kuwa chumvi inaweza kutumika kama kipodozi na kukuacha ukiwa na ngozi nyororo na ya kuvutia?
Kumekuwepo na sababu mbalimbali zinazopelekea warembo kupata matatizo ya ngozi. Kitendo hicho huwafanya warembo husika kupoteza nuru ya ngozi zao na pia matumaini ya kuonekana wenye kuvutia na kupendeza.
Matatizo ya chunusi, ukavu katika ngozi, mafuta usoni na hata mlundikano wa ngozi zilizokufa usoni ni miongoni mwa mambo yanayowakera warembo wengi na hatimaye kupelekea kutumia vipodozi visivyo salama kwa ngozi zao.
Kwa kutambua hilo wataalamu wa urembo wa asili walikuja na njia hii ambayo haina gharama kubwa ukilinganisha na njia zilizozoeleka na warembo wengi.
Matumizi ya chumvi yamekuwa na matokeo mazuri katika matatizo mbalimbali ya ngozi, ingawaje si wengi wanalolifahamu hili.
Unachotakiwa kuzingatia ni kuhakikisha kuwa chumvi hiyo haingii machoni mara utakapoanza kuitumia.
Mahitaji.
Chumvi ya unga kijiko 1 kikubwaNamna ya kufanya
Nawa uso wako kwa maji ya kawaida na kisha chukua kitambaa laini na safi. Chovya kwenye chumvi na kisha sugua katika ngozi yako ya uso taratibu.
Baada ya kupaka katika uso mzima, weka chini kitambaa chako na kisha jisugue kwa kutumia mikono yako. Fanya hivyo hadi utakapoona takataka zinatoka.
Baada ya kufanya hivyo kwa muda wa dakika mbili, osha kwa kutumia maji ya baridi.
Ni muhimu kufanya zoezi hili mara kwa mara kwani bila hivyo krim au losheni yako unayotumia haitafika katika ngozi pindi unapotaka kufanya hiyo.
Unashauriwa kufanya aina hii ya scrub mara moja kwa wiki ili kupata matokeo mazuri.
|