SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Jumapili, 27 Machi 2016

T media news

Rais mteule wa Benin kupunguza muda wa uongozi wa Rais


Rais mteule wa Benin kupunguza muda wa uongozi wa Rais
Rais mteule wa Benin Patrice Talon amesema kuwa, anataka kupunguza muda wa rais anaoweza kuongoza nchini humo, kuwa muhula mmoja tu wa miaka mitano.

Rais huyo mteule wa Benin amesema hayo baada ya Mahakama ya Katiba ya nchi hiyo kuidhinisha ushindi wake wa urais. Bwana Talon, ambaye alimshinda Waziri Mkuu Lionel Zinsou katika duru ya pili ya uchaguzi wa rais juma lilopita amesema kwamba, muda mfupi wa uongozi kwa rais utasaidia kupunguza kile alichoelezea kuwa, tamaa ya Rais ya kutaka kuongoza muda mrefu. Talon alipata asilimia 65.4 ya kura katika duru ya pili ya uchaguzi huo iliyofanyika Jumapili iliyopita na kuibuka mshindi. Rais huyo mteule wa Benin atamrishi Rais Boni Yayi ambaye ameongoza kwa mihula miwili ambapo muda wake wa uongozi unamalizika mwezi ujao. Msimamo wa rais mpya wa Benin ni tofauti na viongozi wengine wa Afrika, ambao hivi karibuni wamekuwa wakiongeza juhudi za kubadilisha katiba na kuendelea kubakia madarakani.