Wapiganaji 60 wa kundi la kigaidi la ash-Shabab nchini Somalia wameuawa mashariki mwa nchi hiyo.
Hayo yameelezwa na afisa mmoja wa polisi nchini Somalia ambaye hakutaka kutaja jina lake kwa sababu za kiusalama na kuongeza kuwa, wanamgambo hao wa ash-Shabab wameuawa katika eneo la Puntland, kaskazini mashariki mwa nchi hiyo ya pembe ya Afrika. Kwa mujibu wa afisa huyo wa jeshi la polisi nchini Somalia, wanamgambo wengine 38 wa genge, wamejeruhiwa. Afisa huyo amenukuliwa akisema kuwa, kutokana na kundi hilo kushindwa na jeshi la nchi hiyo, limewataka wanachama wake kuondoka mjini humo ili kuokoa maisha yao haraka iwezekanavyo. Hadi sasa karibu magaidi 100 wa kundi hilo la kitakfiri wamekwishaua katika operesheni za jeshi la Somalia katika mji huo wa Puntland. Operesheni hizo, zilianza tangu wiki iliyopita na hadi sasa bado zinaendelea katika kuwasaka wanamgambo hao wa ash-Shabab.