ALICHOKIFANYA MISS UBUNGO MCHANA WA PASAKA
“Wape wenye uhitaji, toa ubarikiwe” hiyo ni kwamujibu wa mapokeo ya Biblia, katika pitapita za mchana wa PASAKA T.COM MEDIA imemshuhudia mlimbwende wa Ubungo wa mwaka 2014/2015 Diana Kato akisherehekea #PASAKA yake na watoto yatima na wasio na makazi maalumu wa kituo cha CHAKUWAMA Sinza Jijini Dar es Salaam, kwa kile kidogo alichobarikiwa.
Kimsingi mlimbwende anapokuwa kambini kabla ya kupewa taji la ushindi huwa anafundishwa mambo mengi ikiwemo huduma za jamii lakini huwa inakuwa kinyume baada ya mlimbwende kutangazwa ushindi, jambo ambalo Diana Kato amewakumbusha ‘ma-miss’ kote nchini kutenga muda wao kwa kufanya vitu vya kijamii zaidi.