NEYMAR ATEMWA BRAZIL UNAMJUA MRITHI WAKE?
Na Albogast Benjamin
Mshambuliaji wa Barcelona na mlinzi wa PSG David Luiz wameachwa na timu yao ya taifa Brazil baada ya kusimamishwa kucheza mchezo wa kufuzu Kombe la Dunia dhidi ya Paraguay hivyo kocha wa Brazil Dunga amewaita wachezaji mbadala wa kuziba nafasi hizo mbili.
Kijana Gabriel Barbosa kutoka klabu ya Santos amechukua nafasi ya nahodha wa Selecao Neymar katika kikosi kitakachokipiga na Paraguay.
Neymar alipata kadi ya njano ya tatu mfululizo kwenye michuano hiyo siku ya Ijumaa kwenye sare ya 2-2 dhidi ya Uruguay na atakosa mchezo wa pili wa Brazil dhidi ya Paraguay siku ya Jumanne
Gabriel ameichezea Brazil chini ya miaka 17 , chini ya miaka 20 na chini ya miaka 23, kwasasa ana umri wa miaka 19 na amekuwa akitazamwa na baadhi kama mrithi wa Neymar baada ya kuonesha mkubwa ndani ya Santos.
Naye beki wa Corinthians ya huko Brazil Felipe pia amejumuishwa kwenye kikosi kitakachovaana na Paraguay kufuatia kusimamishwa kwa beki tegemeo David Luiz kwa kuwa na kadi sawa na Naymar.