TIMU YA CHADI ITALIPA FAINI YA DOLA ELFU 20 NA MENGINE YAKO HAP
Na Albogast Benjamin
Shirikisho la soka barani Afrika CAF limetoa tamko rasmi kuhusu kujitoa kwa Chad kupitia Ukurasa wake wa mtandao wa twitter imebainisha kanuni na adhabu itakayo ikuta Nchi hiyo.
Kanuni za chombo hicho kikuu cha soka barani Afrika zinaeleza kuwa endapo timu inayoshiriki ligi inayoandaliwa na CAF ikajitoa bila sababu za msingi basi itatozwa faini isiyopungua dola elfu ishirini pamoja na kufungiwa kushiriki michuano yoyote chini ya CAF kwa takribani miaka miwili.
Kanuni nyingine inayohusu alama zilizopata timu pinzani inaeleza kuwa kama timu ikijitoa katikati ya mashindano basi pointi za timu zote zitafutwa pamoja na magoli ya kufungwa na kufunga yaliyopatikana kwenye michezo dhidi ya timu iliyojitoa.
Kwa maana hii timu ya Taifa ya Tanzania itasalia na pointi moja iliyopatikana kwenye suluhu ya Nigeria kwenye Uwanja wa taifa wakati Nigeria atabaki na alama mbili zilizopatika kwenye sare dhidi ya Tanzania na Misri wakati huo Misri watabaki na pointi 4 wakiongoza kundi G kufuatia ushindi dhidi ya Tanzania na sare dhidi ya Nigeria.
Katika kundi hili Timu itakayoongoza pamoja na atakayeshika nafasi ya pili atapata nafasi ya Kufuzu moja kwa moja kwenye fainali za Afcon mwakani nchini Gabon tofauti na makundi mengine ambayo yatatoa mshindi wa kwanza tu.