Usiku wa kuamkia leo Iran imeshusha mashambulizi makali kwa Israel kwa kupiga uwanja wa ndege wa kimataifa wa Ben Gurion uliopo pembeni ya mji wa Tel Aviv makombora yalionekana yakishuka kwa wingi kama mvua bila mifumo ya ulinzi wa anga wa Israel ku Intercept makombora hayo.
Ben Gurion Airport ni uwanja mkuu wa ndege wa Israel, zaidi ya Asilimia 90% ya wasafiri wa kimataifa wa Israel hupitia hapo, lakini pia ni moja kati ya Airport zenye ulinzi mkali duniani kwani uwanja huo unatumika pia kwa operation za kijeshi na usalama.
Mashambulizi na wingi wa makombora yaliyorushwa usiku wa kuamkia leo Israel umesababisha kutiliwa shaka kwa kauli ya Trump kwa kutangaza ushindi kuwa kaivunja nguvu Iran kwa kuharibu Missile Launchers (mifumo ya kurusha makombora) ya Iran.
Maana ndani ya masaa 24 tangu atoe kauli hiyo Iran wameshambulia maeneo mengi ya mshariki ya kati yenye uhusiano na Marekani, ndani ya masaa 24 Iran wameshambulia Base za marekani kwa kupiga Al-Udair base na Command bulding zilizopo kuwait , baada ya hapo wakapiga US naval infrastructure (miundombinu ya jeshi la wanamaji wa marekani) huko Bahrain, lakini pia wakapiga oil facilities ikiwepo Bapco ,Oild depots ya Kuwait na Oil refinery ya Haifa huko Israel.
Na baada ya hapo ndipo usiku wa kuamkia leo Iran wakatangaza Supreme Leader mpya ambae ni Ayatollah Mujtaba Khamenei na wakamkaribisha kwa kuishambulia Israel kwa makombora mengi maeneo mbalimbali ikiwepo uwanja huu wa Ben Gurion.
Je kwa idadi ile ya makombora waliyorusha jana Iran ni kweli Trump aliharibu mifumo ya kurusha makombora (Missile Launchers) za Iran au hana taarifa za uhakika kuhusu nguvu ya Iran?
