HABARI SANAA NA MICHEZO

Jumatatu, 9 Machi 2026

T media news

Raisi wa Marekani Donald Trump amempongeza waziri mkuu wa Australia Anthony Albanese kwa kitendo cha Australia kuwapa hifadhi wachezaji wa timu ya Taifa ya mpira wa miguu ya Iran


 ambao wanayahofia maisha yao endapo watarudi nchini Iran 


Trump amempongeza Albanese kwa kitendo hicho cha kiungwana cha kuwa hifadhi wachezaji hao ambao wengine wanataka kurudi nchini Iran wakidai kuwa endapo wasiporudi serikali ya Iran itaziumiza familia zao 


Siku ya tarehe 2 mwezi huu baadhi ya wachezaji wa timu ya Taifa ya wanawake ya Iran waligoma kuimba wimbo wa Taifa lao wakati wa ufunguzi wa mechi ya mpira wa miguu kati ya timu ya Taifa ya Iran na Korea kusini  mechi ya mashindano ya Asia women's Cup


Wachezaji hao waligoma kuimba wimbo huo ikiwa ni ishara yao ya kuipinga serikali ya Iran ambayo wakati huo tayari ilikuwa imeshaingia vitani na Marekani na Israel 


Baada ya mechi hio ambayo timu hio ya Iran ilifungwa bao 3-0 hao walikataa kurudi nchini Iran wakidai kuwa serikali ya Iran imewaona kama wasaliti na hivyo maisha yao yapo hatarini, huku baadhi wakidai kuwa familia zao zilizopo nchini Iran zinatishiwa maisha endapo wao hawatorejea


Wachezaji 5 wa timu hio walitoroka kambi na kukimbilia kwenye mamlaka za Australia kwaajili ya usalama wao ambapo kwasasa wanalindwa na vyombo vya usalama vya Australia , wachezaji wengine bado wapo nchini humo nao wakiwa chini ya ulinzi kuepuka kufanyiwa chochote