Habari sanaa na michezo

Jumatatu, 9 Machi 2026

T media news

Rais wa Urusi, Vladimir Putin amesaini na kurasimisha sheria inayokataza kuwarejesha (Extradition) raia wa kigeni waliotumikia na wanaotumikia Jeshi la Urusi.

Kwa maana hii, wageni au watu wasio na uraia (stateless) hawatarejeshwa nchini mwao au nchi yoyote kwa ajili ya kufunguliwa mashtaka ya jinai kwa kushiriki vita vya Urusi na Ukraine, badala yake watasalia nchini Urusi na kupewa uraia. 

 Sheria hii inawalenga wale wanaotumikia sasa na waliowahi kutumikia huko nyum kwa mkataba katika jeshi la Urusi au katika “vikosi vingine vya kijeshi” vya Urusi.



Bunge la Urusi, State Duma, liliidhinisha sheria hiyo mnamo tarehe 26 Februari 2026 na baadaye Baraza la Shirikisho la Urusi (Federation Council of Russia) likaipitisha tarehe 4 Machi 2026. 


Kabla ya sheria hii wageni walipewa haki ya kusaini mikataba ya kujiunga na jeshi la Urusi kuanzia Novemba 2022, na baadaye Julai 2024 watu wasio na uraia rasmi nao walirubusiwa. 


Kwa mujibu wa Alexander Bastrykin, mkuu wa Kamati ya Uchunguzi katika jeshi la Urusi alisema kufikia Januari 2024 takribani wahamiaji 10,000 waliokuwa na uraia wa Urusi tayari walikuwa wameshiriki katika operesheni ya kijeshi nchini Ukraine. 

Na kuanzia hapo, wageni wengine waliotia saini mikataba ya kuhudumu katika jeshi la Urusi kabla ya kumalizika kwa operesheni ya kijeshi nchini Ukraine, pamoja na wanafamilia wao, wanaweza kupata uraia wa Urusi kupitia mchakato rahisi zaidi baada ya Rais Putin kusaini sheria hii. 


Hakutakuwa na ulazima wa kutimiza sharti la kuishi nchini Urusi kwa miaka mitano ili kupata kibali cha makazi ya kudumu.

Wale watakaoachishwa kazi jeshini na hata waombaji ambao watathibitika kuwa hawana vigezo vya kuhudumu jeshini, nao pia wanaweza kuomba uraia wa Urusi kupitia mchakato uliorahisishwa na sheria hii.