HABARI SANAA NA MICHEZO

Jumapili, 8 Machi 2026

T media news

NEW DELHI: Muigizaji mkongwe na mwanasiasa Kamal Haasan (71) amejibu kwa ukali kauli kutoka kwa utawala wa Donald Trump


  Kuhusu ununuzi wa mafuta ya Urusi kwa taifa la India, akimwambia Rais huyo wa Marekani “ashughulikie mambo yake mwenyewe” huku akitetea haki ya India kama taifa huru kuamua sera yake ya nishati.


Katika ujumbe aliouchapisha kwenye mtandao wa X na kumuelekeza moja kwa moja kwa Rais wa Marekani, Kamal Haasan alisema suala hilo linahusu uhuru wa taifa na kuheshimiana kati ya nchi.

“Sisi watu wa India ni wa taifa huru na lenye mamlaka kamili. Hatupokei tena amri kutoka nchi za mbali za kigeni. Tafadhali shughulika na mambo yako mwenyewe kadiri uwezavyo. Kuheshimiana kati ya mataifa huru ndio msingi pekee wa amani ya kudumu duniani.” aliandika Kamal Haasan.


Hayo yamejiri baada ya Donald Trump kutoa maelekezo kwa India kuwa wasinunuwe mafuta kutoka Urusi kwani ndio taifa linalo nunua mafuta mengi sana kutoka nchi hiyo kuliko nchi nyingine nyingi duniani. 


Aidha, Kamal Haasan alimalizia ujumbe wake kwa kuitakia Marekani na wananchi wake mema kwa kusema... “Tunalitakia taifa lako na wananchi wake amani na mafanikio.


Kamaal Hasaan Anajulikana zaidi kupitia filamu kama vile... Geraftaar, Saagar, Vikram, Indian, Chachi 420, Mumbai Express, Kalki 2898 AD, Indian 2, Thug Life na nyengine kibao ambazo hazijatajwa hapo.