Habari sanaa na michezo

Jumapili, 8 Machi 2026

T media news

Katika kilele cha Siku ya Wanawake Duniani, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, amemzawadia mama mzazi wa marehemu Steven Kanumba gari jipya aina ya Harrier New Model.




Hatua hii imekuja kama ishara ya kuthamini mchango mkubwa wa marehemu Kanumba katika kukuza tasnia ya filamu nchini na kuenzi alama aliyoiacha kwenye sanaa ya Tanzania.


Zawadi hiyo ni jibu la ombi la Mama Kanumba kwa Rais Samia, ambapo alieleza changamoto ya usafiri inayomkabili kutokana na umri wake mkubwa. 


Akishukuru kwa furaha, Mama Kanumba amempongeza Rais kwa moyo wa upendo na ukarimu, akibainisha kuwa usafiri huo utamsaidia kurahisisha shughuli zake za kila siku ambazo awali zilikuwa ngumu kwake.