SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Jumatano, 11 Aprili 2018

T media news

Makonda ataja sababu zilizompelekea kuwasaka wanaume waliotelekeza watoto

Mkuu wa Mkoa wa Dar es SAlaam, Paul Makonda ameeleza kuwa, yeye kuanzisha kampeni ya kuwasaidia kina mama waliotelekezwa na waume zao, kumetokana na sababu mbali mbali ambazo amezifanyia utafiti kwa muda mrefu.

Akizungumza jana katika mahojiano na mtangazaji wa Azam TV, Chars Hillary, Makonda amesema kuwa kumekuwepo na mapungufu mengi katika mamlaka husika zinazoshughulikia masuala ya wanawake na watoto, jambo ambalo limepelekea kushindikana kutatuliwa kwa kesi hizo.

Paul Makonda amesema kuwa ofisi yake imekuwa ikipokea malalamiko mengi kutoka kwa wanawake mbalimbali, jambo lililompelekea yeye kutafuta njia bora zaidi ya kulitatua tatizo hilo linaloonekana kuwa kubwa katika jamii.

“Tumekuwa na wananchi wanaofika kwenye ofisi ya Mkuu wa Mkoa, moja kama maelekezo ya Rais Magufuli ya kusikiliza na kutatua kewro za wananchi. Kwa hiyo mimi nimeanza utafiti mwezi wa pili kwamba, kulikoni wakinamama wengi wana changamoto za namna hiyo.”

“Mojawapo nikaanza kuziangalia mamlaka husika ambayo ni Ustawi wa Jamii. Nikaona kuna tatizo la pande zote mbili,” amesema Paul Makonda.

Akizungumzia upande wa mamlaka, Makonda ameeleza kuwa wanawake wanapofika Ustawi wa Jamii, wapo baadhi ya wanaume kutokana na sababu zao binafsi hutumia fedha kuhonga ili kesi zilizowasilishwa na wanawake zibadilishwe.

“Wakati nahangaika pia katika utafiti wangu, nikaja kubaini wengie wakienda kwenye viuo vya ustawi wa jamii, wakiitwa wanaume wanahonga pesa kwa baadhi ya mamlaka na wanabadilishiwa kesi wale kinamama kwamba wanataka kuwadhalilisha wale kina baba. Jambo ambalo linawaogopesha kina mama kujitokeza kwenda kwenye mamlaka,” amesema Mkuu wa Mkoa wa Dar, Paul Makonda.

Alipoulizwa kama zoezi linaloendelea lina mantiki yoyote kisheria, Makonda alijibu kuwa “Ipo, imekaa vizuri sana na Bunge letu lilitunga sheria nzuri sana. Ndiyo maana tunaanza na reconciliation (makubaliano). Tunakaaa mezani na baab na mama wa mtoto tunakubaliana. Ikitokea mwanaume amekataa basi ndipo tunasogea kwenye hatua ya DNA. Na bahati nzuri katika ofisi yangu nina wataalamu kutoka kwa Mkemia Mkuu wa Serikali.”

Hata hivyo, zoezi hili limeanza kuonyesha mafanikio kwani baadhi ya wanaume wameshapokea barua za wito kufika katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar ili kufanya mazungumzo kuhusiana na malalamiko yaliyowasilishwa na wanawake wanaodai kuwa wamewatelekeza.

Hapa chini ni mfano wa barua ya wito.