Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) limetoa taarifa kwa umma kuhusu kukatika kwa umeme usiku wa kuamkia Jumamosi ya Machi 10 katika mikoa iliyounganishwa kwenye gridi ya Taifa.
Taararifa ya Tanesco imeeleza kuwa majira ya saa 8:49 usiku kumetokea hitilafu katika mfumo wa gridi ya Taifa iliyopelekea kukosekana kwa huduma ya umeme katika maeneo na mikoa yote iliyoungwa kwenye gridi ya Taifa.
Baada ya hitilafu hiyo kutokea, mafundi na wataalamu wa shirika hilo walichukua hatua za haraka na bado wako kazini kuhakikisha kuwa huduma ya umeme inarejea mapema kadri iwezekanavyo.
Uongozi wa shirika hilo umeomba radhi kwa usumbufu uliojitokeza lakini ukitoa tahadhari kwa wananchi kuwa wasishike wala kukanyaga ulioanguka au uliokatika ili kuepusha madhara zaidi.