Kuna msemo wa kiswahili unaosema kuwa, kuishi kwingi ni kiuno mengi. Huo unaweza ukawa msemo sahihi kuilezea tukio hilo la mtoto wa miaka mitano aliyemfikisha baba yake katika Kituo cha Polisi Ngara mkoani Kagera kwa kile alichoeleza kuwa alitaka kuuza shamba kinyemela.
Video ya mtoto huyo ambae jina lake halikuweza kufahamika mara moja, alisema kwamba alilazimika kwenda Polisi baada ya kubaini kuwa baba yake mzazi ameingia makubaliano na mtu mwingine ili auze shamba ambalo wamekuwa wakilitumia.
Mtoto huyo anayekaridiriwa kuwa na umri wa miaka 5, alisema baba yake alipanga kuuza shamba hilo bila kushirikisha wanafamilia wengine, hali ambayo yeye hakifurahia.
Uwezo wa mtoto huyo ndio umekuwa kivutio miongoni mwa wengi kutokana na namna anavyoonyesha uelewa wa mambo, lakini pia uwezo wake wa kujibu maswali.
“Anataka kuuza shamba, sasa tutaishi wapi?” alihoji mtoto huyo alipokuwa akiulizwa na watu kwanini amemshtaki baba yake mzazi.
Alisema kuwa mtu aliyefahamika kwa jina moja la Thabiti alimpa lifti kutoka kijijini kwao Kabanga, wilayani Ngara hadi kituo cha Polisi ambapo alipatiwa msaada. Polisi walimchukua mtoto huyo na kurudi nae hadi nyumbani kwao, kisha kuzuia baba wa mtoto huyo asiuze shamba
“Polisi walikuja wakamuuliza baba kama kweli anataka kuuza shamba, baba akasema hajauza, wakataka kumpeleka kituoni nikakataa…” alieleza mtoto huyo.