SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Jumatano, 21 Februari 2018

T media news

Sakata la Kumfukuza Miguna Lachukua Sura Mpya ....... Serikali, Mahakama Zavutana

Sakata la kumfukuza nchini mwanasheria maarufu wa kenya Miguna Miguna linazidi kuchukua sura mpya baada ya mahaka Kuu kuamuru arudishwe nchini mara moja.

Jaji Luka Kimaru ameamuru Dkt Miguna arudishwe Kenya kwa kuwa Serikali ilikaidi agizo la mahakama, la kutakiwa kufikishwa mahakamani kwa mwanasheria huyo baada ya tukio la kumuapisha Raila Odinga.

Jaji Kimaru amesema hatua ya serikali kumfukuza Miguna ni kinyume cha katiba na sheria za kimataifa na kwamba mtu moja hawezi kupokonywa uraia wake.

Miguna ni mzaliwa wa eneo la Nyando, kaunti ya Kisumu lakini alipata uraia wa Canada alipoenda kusoma elimu ya juu na kuanza kufanya kazi za sheria.

Kwa upande wa serikali imesema ilipasa kumchukulia hatua hiyo Miguna baada ya kupata taarifa kutoka kwa usalama wa Taifa, kuwa mtu huyo ni hatari kwa usalama wa nchi.