SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Jumatano, 21 Februari 2018

T media news

Inasikitisha! Mtoto wa Miaka Sita Afariki Baada ya Kupelekwa Mlimani Kutolewa Mapepo

 Mtoto wa miaka sita amefariki dunia akiombewa mlimani alikopelekwa kutolewa mapepo, huku mama yake mzazi akishikiliwa polisi.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita, Mponjoli Mwabulambo akizungumzia tukio hilo amesema lilitokea Februari 18,2018 saa tano asubuhi katika mlima Gambiwe.

Amesema mama wa mtoto Neema Petro (25) na mke mwenzake Raheli Musa (25) walikwenda mlimani na mtoto huyo kwa ajili ya maombi na kufunga.

Kamanda amesema wanawake hao wakazi wa kijiji cha Bukulu wilayani Nyang'hwale wanashikiliwa kutokana na kifo cha mtoto Frank Bariki (6), ambaye mwili wake umekutwa na majeraha shingoni na kwenye mbavu.